Baada ya kumaliza mkataba na timu yake ya TP-Mazembe na kupitia kipindi kifupi cha sintofamu iliyowapa shaka wapenda soka wengi nchini Tanzania, mchezaji Thomas Ulimwengu amesajiliwa nchini Swiden.
Timu hiyo ya AFC Eskilstuna iliyopanda daraja msimu huu imeongeza jina la Ulimwengu katika safari ya kwenda Hispania kesho watakapoweka kambi ya miezi miwili kwa ajili ya maandalizi ya ligi kuu nchini Swiden inayotarajiwa kuanza Aprili 1, 2017.
Ulimwengu amesaini mkataba wa miaka miwili na timu hiyo na Watanzania wengi wanatarajia ataiwakilisha vyema nchi yetu kama anavyofanya swahiba wake waliokuwa pamoja TP Mazembe, Mbwana Samatta katika klabu ya FC Genk ya nchini Ubelgiji.
Post a Comment
Post a Comment