Rais John Pombe Magufuli leo tarehe 1/1/ 2017 ametengua uteuzi uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba na kumteua Dk Tito Esau Mwinuka kuwa Kaimu Mkurugenzi wa shirika hilo.
Akiwa mkoani Kagera leo Rais Magufuli alisikika akisema kuwa haiwezekani mtu mmoja kutokana na nafasi yake afanye maamuzi ya kupandisha umeme huku akitambua kuwa kufanya hivyo ni kuwaumiza watanzania na kuahidi kuendelea kuwatumbua wafanyakazi wa Serikali ambao ni majipu.
Post a Comment
Post a Comment