Stela (38) aliyekuwa mkazi wa Manispaa ya Shinyanga ameuawa na mumewe kwa kosa la kutohifadhi kachumbari, kitendo kilicho sababisha iharibike.
Habari hii imethibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Elias Mwita na kusema kuwa jeshi la polisi linamshikilia mtuhumiwa ambapo uchunguzi wa awali umebaini jeraha katika utosi wa marehemu lililosababishwa na ugomvi wa kifamilia.
Watoto wa marehemu waliwaambia waandishi wa habari kuwa kabla ya kuanza kumpiga, baba yao alihoji kwa nini kachumbari aliyokula na kubakiza jana yake ilikuwa imechacha. “Baba alirudi nyumbani saa moja jioni na kutuagiza tumletee kachumbari aliyobakiza jana yake”. Alisema mtoto mmoja.
Watoto hawa waliadhibiwa na kufanikiwa kukimbilia nje ya nyumba. Muda mfupi baadae mama yao akarejea na kumkuta mumewe akiendelea kugombea. “Mama alirejea na kupokewa kwa maswali na kipigo kwa nini kachumbari imechacha” aliongeza.
Walisema baba yao alimpiga kwa mateke na kuchukua kikombe kilichokuwa karibu yake na kumpiga nacho na kumuona mama yao akianguka chini kitendo kilichowafanya kukimbilia kwa majirani kuomba msaada.
HT – Mwnanchi.
Post a Comment
Post a Comment