Mmoja wa watoto wa wafalme Uarabuni amefanya jambo hilo lililozua gumzo baada ya picha iliyosambaa mtandaoni ikionesha ndege hao wakiwa wamewekwa sawa na abiria. Picha hii ilichapishwa katika mtandao wa ‘Reddit’ na mtu anayejiita lensoo ambapo alisema kuwa ametumiwa picha hiyo na rafiki yake ambaye ni rubani wa ndege.
Picha hii inaonesha ndege aina ya mwewe wakiwa wamepandishwa ndege, jambo liliozua mjadala mkubwa kwenye mtandao wa Reddit
Mtu huyo alisema kwamba mwewe 80 walipandishwa ndani ya ndege wakiwa wamefungwa mbawa zao ili wasiweze kuruka wakiwa ndani. Ingawa haijathibitishwa bado, lakini inaaminika kuwa mwewe hawa walisafirishwa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Qatar.
Shirika la Ndege la Etihad pia linaruhusu kusafirisha ndege ambapo kwenye tovuti ya shirika hilo wameandika, Tunakubali kusafirisha mwewe na tai ndani ya ndege kama abiria ikiwa tu nyaraka zote zinazotakiwa zikioneshwa. Pia tunakubali ukitaka kuwasafirisha kama kifurushi cha mzigo.
Tai ni moja ya nembo za Umoja wa Falme za Kiarabu ambapo wanaruhusiwa kuwa na hati za kusafiria (passport) kwa ajili ya ndege, hii ikiwa moja ya mipango ya kuzuia usafirishaji haramu wa ndege hao.
Post a Comment
Post a Comment