const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); MDUKUZI (HACKER) ALIYEDUKUA AKAUNTI 500 YA ISIS TWITTER, ATUMA UJUMBE KWA TRUMP - HABARI MPYA

..

MDUKUZI (HACKER) ALIYEDUKUA AKAUNTI 500 YA ISIS TWITTER, ATUMA UJUMBE KWA TRUMP


Mdukuzi (Hacker) aliyedukua akaunti 500 za kundi la kigaidi la Dola la Kiislamu (ISIS) ana ujumbe kwa Rais Donald Trump wa Marekani ambapo amemtaka kuimarisha ulinzi wa akaunti zake za Twitter mapema iwezekanavyo.

Kwa mijibu wa mdukuzi huyo anayefahamika mitandaoni kwa jina la WauchulaGhost, Rais, Makamu wa Rais na Mke wa Rais wapo katika hatari kubwa ya akaunti zao kudukuliwa kwa sababu ya ulinzi wake kutokuwa imara.

Mapema Jumatatu Januari 23, WauchulaGhost alichapishwa barua pepe (emails) zinazohusiana na akaunti za viongozi hao na kuwataka kuzibadilisha na pia kuimarisha ulinzi kwani akaunti zao za Twitter ni rahisi mno kudukua. Alisema barua pepe zilizotumiwa kwenye baadhi ya akaunti hizo ni rahisi sana kuzijua kwani ilimchukua dakika 20 tu kujua barua pepe ya Makamu wa Rais ([email protected]) kuwa [email protected]

Mwezi Juni mwaka jana, WauchulaGhost aligonga vichwa vya habari duniani baada ya kudukua akaunti500 za ISIS na kisha kuchapisha picha za utupu na jumbe za watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Akitolea ufafanuzi kuhusu akaunti za viongozi hao wajuu wa Marekani (@POTUS, @FLOTUS na @VP) WauchulaGhost alisema hawajaweka barua pepe na namba za simu zitakazohitajika kama mtu atakuwa amesahau nywila (password) hivyo ni rahisi kwa yeyote kuingia kwa kusema amesahau nywila na akawezeshwa kubadilisha.

Mdukuzi huyo alisema kuwa hana lengo la kuzichukua akaunti hizo lakini amewapa tahadhari kwa sababu zipo katika hatari.

Related Posts

Post a Comment