Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na mbunge wa Hai, Freeman Mbowe amekiri kuwa yupo katika hali tete na kuwa inamuwia vigumu kuendesha kampuni yake ya Free Media ambayo huchapisha gazeti la kila siku la TanzaniaDaima.
Kwa mujibu wa habari iliyochapishwa kwenye gazeti la Uhuru la Januari 07, 2017 Mbowe amepunguza idadi ya wafanyakazi katika kampuni yake na wamebakia 14 baada ya kushindwa kuwalipa mishahara yao na stahiki nyingine.
Aidha, imeelezwa kuwa wafanyakazi hao wamelalamikia njia iliyotumika kuwafuta kazi na kwamba ni ubabe kwani awali walichukuliwa kutoka katika kampuni nyingine na kuwalaghai ili awatumie katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Sakata hilo limepelekea Mhariri Mtendaji wa Free Media, Naville Meena kujiuzulu na nafasi yake kukaimiwa na Martin Mlela. Mbali na huyo, Meneja Rasilimali Watu na Utawala, Vaileth Temba na Meneja Matangazo na Biashara, Twalib Mungulu na jana walikabidhi barua za kuachia ngazi.
Habari hiyo iliendelea kueleza kuwa kikao alichofanya Mbowe na Wahariri na waandishi wanne aliwaambia kuwa atafanya mabadiliko ikiwa ni pamoja na kupungaza wafanyakazi na kushusha kima cha mshahara.
Kabla ya kikao hicho kufanyika wafanyakazi walikusudia kugoma wakishinikiza kulipwa stahiki zao lakini waliombwa kutofanya hivyo na kuwa wangelipwa madai yao yote. Hadi kikao kinafanyika hawakuwa wamelipwa na majina yalibandikwa ambapo ambao hawakuona majina yao ndio ulikuwa mwisho wa kazi.
Wafanyakazi wengine walidai kuwa malipo yao hayakuwa yakipelekwa NSSF na hivyo kusababisha wao kukosa huduma muhimu ikiwemo fao la kujifungua.
Post a Comment
Post a Comment