const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); KAMANDA MPINGA AMLIPISHA FAINI TRAFIKI - HABARI MPYA

..

KAMANDA MPINGA AMLIPISHA FAINI TRAFIKI

Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani, Mohammed Mpinga ametaka wananchi wanaotozwa faini za makosa barabarani kinyume na makosa husika kuwasilisha malalamiko yao kwake ili askari waliofanya kitendo hicho wachukuliwe hatua kwani jambo hilo halikubaliki na kusisitiza kuwa kila anayefanya kosa anapaswa kutozwa faini kulingana a kosa husika, si kulazimishwa alipe faini hata kama hajafanya kosa huku gari lake likiwa halina tatizo.

Ufafanuzi huo umekuja takribani siku tatu baada ya mkazi wa Dar es salaam kukamatwa na askari akidaiwa kuweka kioo cha giza (tinted) kwenye gari lake, lakini alipofikishwa kituoni ikabainika aliweka kipande kidogo kwenye kioo cha mbele ili kuzuia mwanga wa jua.

Kamanda huyo aliandika kwenye mtandao wa kijamii, “Nilimwita yule askari na kumweleza kuwa alichokifanya si sahihi na kumtaka alipe faini aliyoiandika.”

“Iko tabia ya baadhi ya watu kulazimishwa kuandikiwa kosa. Madereva wengi wakiona wametendewa jambo ambalo hawajaridhika nalo hawapendi kuona viongozi wakati namba zetu zipo,” alisisitiza. Kumekuwa na mvutano kati ya trafiki na madereva wanaokamatwa kwa makosa mbalimbali, ambapo wengi wanalalamika kuonewa kwa kubambikiwa makosa.

Kamanda Mpinga amesema pia kwa sasa wapo katika mchakato wa kubadili faini za makosa ya usalama barabarani yenye lengo la kuongeza faini hizo kutoka shilingi 30,000 za sasa. Alisema uamuzi huo utasaidia madereva kupunguza makosa kwa kuhofia kutozwa faini kubwa kwani wapo wanaofanya makosa yale yale kwakuwa wanajua hata wakitozwa faini watamudu kulipa.

Related Posts

Post a Comment