Muendelezo juu ya ubora fulani ambao mwanadamu anaweza kuwa nao katika kipindi fulani cha maisha yake ni jambo linalohitaji nidhamu,weledi, kujituma na utayari wa mtu kujifunza na kukubali kufanyia kazi mapungufu anayokuwa nayo.
Nchini kwetu suala la mtu kuweza kutunza ubora fulani aliokuwa nao katika jambo fulani ni mtihani mzito kweli kweli. Mara ngapi tumeona waigizaji, wanamuziki,wanamichezo, wanasiasa,hata watu wa kawaida,wakionyesha ubora fulani na baada ya kipindi kifupi tu wakashuka kwa kasi ya ajabu kama si kupotea kabisa?
Kwahiyo inapotokea kuna mtu kaonyesha kuutunza ubora wake kwa kipindi kirefu basi haina budi kutoka hadharani na kumpa sifa zake. Sote watu wa jamii ya muziki tunamfahamu Prince Dully Sykes, ukipenda mwite Mr Misifa. Ana kila sababu ya kusifiwa hasa ikikumbukwa ni mmoja ya watu wa mwanzo kuanza kufanya muziki lakini mpaka leo yupo anarindima kwenye ramani ya muziki.
Hii haitokei tu,Ila ni utayari wake wa kubadilika kulingana na mahitaji ya muziki kwa wakati husika,kukubali kujifunza hata kwa wadogo zake aliowakaribisha kwenye muziki. Lakini kujituma na ubunifu kila uchwao
Analowashindia wasanii wengi wakongwe wao kila kukicha ni lawama na maneno ya kuamini wasanii wa sasa wanaupoteza na kuuharibu muziki na kuamini wadau na media wanawabeba. Lakini Dully ameamua kuamini kua muziki unabadilika kulingana na mahitaji ya wakati husika.
Binadamu hata awe na ubora na kipawa kiasi gani mwisho wa kujifunza kwake ni pale pumzi yake ya mwisho inapokata. Ili uweze kudumu katika jambo lolote lazima uone msingi wa hayo yote ni kujifunza hata kwa wale unaowaona ni wadogo kwako.
Salute kwako Dully Sykes bila kuwasahau Lady Jaydee, AY, Fid Q, Mr Blue, Mwana FA na wengineo waliokuwepo juzi, jana na mpaka leo na wapo wanalisongesha game.
Post a Comment
Post a Comment