Uongozi wa klabu ya soka ya Yanga unakanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa uongozi "umemtimua" kocha mkuu Bw George Lwandamina.
Taarifa hizo sio za kweli tunaomba wanachama na mashabiki wetu mzipuuze zimekaa "KIMATOPENI ZAIDI"
Bado George Lwandamina atabaki kuwa kocha mkuu wa Yanga kwa muda wote wa mkataba wake.
Imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga Makao makuu.
12/01/2017
MKIA NI MKIA TU . . . . . KAMWE HAUWEZI KUWA USO!
Baada ya kuona Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Tanzania, na mabingwa wa kihistoria wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa imara, bila kuteteleka wala kubabaika kutokana na ushindi wa matuta ya viazi mviringo, mkiani badala ya kujipanga mechi yao na Lambwa Lambwa, wao wakaamua KUPIKA MAJUNGU KUPITIA GROUP LAO LA WHATSAPP (Nitaliweka hapa muda si mrefu) kwamba Mabingwa wa Nchi wameachana na Super Coach GL.
Ugonjwa wao wa kutokubali matokeo, kufanya vurugu, kuvunja na kuharibu viti, na sasa kulilia refa wa nje, wanadhani watawaambukiza Wananchi wanaojielewa wa Jangwani.
MBAYA ZAIDI, wanatumia mikia wenzao wenye ajira kwenye magazeti na redio mbalimbali nchini kusambaza habari zao za kimikia mikia.
Kwa vile wao wanachanganyikiwa na kupagawa akili kila wanapobamizwa, tofauti na sisi Wananchi ambao tunakuwa waungwana na kukubali matokeo, basi WANAUMIA SANA WANAPOONA HATUNA TABIA ZA MIVURUGANO KAMA ZAO.
HICHI NDICHO KINACHOWAUMA MIKIANI . . . !! MUDA SI MREFU TUTAWAANIKA HADHARANI MIKIA WOTE (TENA VIONGOZI WAO) WALIOPIKA HIZI HABARI.
- Ngariba HAOGOPI MKOJO, NGOJA TUWAKATE TU . . . .
Post a Comment
Post a Comment