News
Njombe
Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka ameshuhudia zoezi la utiaji saini wa mikata ya ujenzi wa mtambo wa kutibu maji kutoka chanzo cha mto Mbukwa wilayani Wanging'ombe pamoja na mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji katika kata ya Mlowa mjini Makambako mkoani Njombe yenye thamani ya shilingi bilioni 6.7 ili kukabiliana na changamoto ya maji kwenye maeneo hayo.
Mtaka amemuagiza mkandarasi wa miradi hiyo inayokwenda kutekelezwa na kampuni ya Patty Interplan ltd kwenda kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria endapo miradi hiyo itashindwa kutekelezwa kulingana na matakwa ya mkataba.
"Huyu bwana (OCD) yuko hapa amekuja kushuhudia vizuri tu halafu kesho itabidi ageuke akuweke pingu kukupeleka lock up lakini leo tumekuja hapa tumeshangilia na kushikana mikono"amesema Mtaka
Aidha Mtaka amemuhakikishia ushirikiano mkubwa mkandarasi kwenye kila hatua za utekeleaji wa miradi hiyo huku akiadi kuwa nae bega kwa bega kwenye miradi mingine endapo miradi hiyo itatekelezwa kwa ufanisi kwa kuwa yeye ni mdau mkubwa wa wakandarasi wazawa.
Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo Mhandisi Oscar Lufyagile ambaye ni mkurugenzi wa mamlaka ya maji mjini Makambako (MAKUWASA) amesema miradi hiyo itawanufaisha wananchi wapatao 61,739 ambapo kwenye eneo la Makambako jumla ya wananchi 6,659 na taasisi kama vile kiwanda cha kutengeneza mipira ya mikono na dawa eneo la Idofi,Hospitali ya mji wa Makambako na shule za msingi na sekondari zilizopo kwenye kata ya Mlowa.
Katika eneo la Wanging'ombe amesema wananchi 55,080 katika kata 10 za Igwachanya,Ilembula,Usuka,
Kwa upande wake mkurugenzi wa Patty Interplan ltd Patrick Mbedule ameahidi kutekeleza ujenzi wa miradi hiyo kulingana na matakwa ya mikataba huku pia akiomba ushirikiano mkubwa wa serikali na wananchi katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Post a Comment
Post a Comment