KERO za Michango ya Sherehe Katika Jamii ya Watanzania

Wakuu hii kitu bado bongo ipo tena siku hizi ni project kubwa na za garama ya juu.

Watu wanakutana kila wiki mara moja kwenye baadhi ya bar, wanakunywa na kusaza katika hivyo vikao vya maandalizi, vikao hivyo huchukua miezi miwili hadi mitatu. Na katika vikao hivyo watu hutoa ahadi ya kiasi cha fedha watakachotoa kwa ajili ya harasi, wanaume hutoa michango ya bachela parti na harusi kuu, na kina dada hutoa michango ya sendi off, bridoshawa, kichenipati, na harusi kuu.
 
Kwa kifupi zoezi hili linakula hela nyingi sana, nimeambiwa sometimes you can be asked to contribute to more than 10 wedding a year, na ukitoa chini ya laki moja unaonekana mtu wa hovyo hovyo.

Jamani ndugu zangu naombeni mwongozo mimi naona kama hii ni too much. Badala ya michango ya vikao vya harusi basi tuihamishie kwenye Elimu na Matibabu.

Related Posts

Post a Comment