Baada ya kupewa adhabu ya kufungiwa kujihusisha na shughuli za sana kwa muda wa miezi sita na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, msanii Suzan Michael ‘Pretty Kind’ amesema kuwa ana mpango wa kuhamia nchini India ambako alikuwa anaishi awali.
Pretty Kind ambaye alipewa agizo la kutojishughulisha na shughuli za sanaa kwa muda wa miezi sita na Naibu Waziri wa WQizara hiyo, ameeleaz kuwa haoni faida ya kuendelea kuwepo bongo kwa kipindi hichi cha adhabu, akihofia kuchekwa na watu.
Mlimbwende huyo ameeleza kuwa kwa sasa anarudi nchini india kwa mwandani wake alikokuwa kiishai awali, ambapo atakuwepo mpaka pale adhabu yake itakapoisha.
Mlimbwende huyo ameeleza kuwa kwa sasa anarudi nchini india kwa mwandani wake alikokuwa kiishai awali, ambapo atakuwepo mpaka pale adhabu yake itakapoisha.
“Ni kweli najiandaa ‘soon’ naenda India, maana masharti niliyopewa ni magumu mno kuambiwa hata picha nisiweke mtandaoni imeniuma sana, ili nitii vizuri hili agizo nimeona bora nisiwepo hapa nchini, adhabu ikiisha nitarudi.” Alisema Pretty kind.
Post a Comment
Post a Comment