const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); FAIDA ZINAZOPATIKANA WATOTO KUNYONYA VIDOLE - HABARI MPYA

..

FAIDA ZINAZOPATIKANA WATOTO KUNYONYA VIDOLE

Ripoti mpya inasema watoto wanaonyonya vidole au kung’ata kucha zao kwa meno huenda wasipate matatizo ya kuathirika kutokana na mazingira hewa au kula vyakula fulani.


Unyonyaji wa kidole gumba na ung’ataji wa kucha umeonekana kuzuia baadhi ya alergy. Watoto wanaoweza kupata matatizo ya kuathirika kutokana na mazingira hewa au kula vyakula fulani (alergy) kutokana na vitu kama vumbi kutoka majumbani, manyoya ya paka au mbwa lakini watoto wenye kunyonya vidole gumba na kung’ata kucha walikuwa ni chini ya theluthi moja kuliko watoto wenye tabia hii ya unyonywaji vidole.
Image result for WATOTO WANAONYONYA VIDOLE

Kati ya watu 1,000 wenye umri wa kati ya miaka mitano hadi thelathini na mbili walifanyiwa uchunguzi kwa muda nchini New Zealand na majibu ya utafiti huo kuonyesha kuwa unnyonyaji vidole una faida kwa watoto.

Tabia hii ya unyonyaji vidole na ung’ataji kucha haisaidii watu wenye pumu au mtu anapopata homa kali.

Uchunguzi uliofanywa na kurekodiwa kwa watoto wenye umri wa kati ya miaka 5 na 11 na wengine waliofanyiwa vipimo ni wenye umri kati ya miaka 13 na 32 (wote wakiwa wanapenda kunyonya vidole) na majibu kuonyesha kuwa wameonekana kuwa wana kiwango kidogo cha kuathirika kutokana na mazingira hewa au kula vyakula fulani.


Tabia hii ya unyonyaji vidole au ung’ataji kucha inaonekana kuwa kinga mpaka wanapofikia umri wa utu uzima.

Kuwa na paka au mbwa majumbani,ndugu au jamaa wanaofanya kazi mashambani pia imeonekana kuwa ni sababu kubwa inayosababisha mazingira ya ukuaji wa magonjwa yanayosababishwa na kuathirika kutokana na mazingira hewa au kula vyakula fulani.
Je, wewe ulikuwa unapenda kunyonya kidole/vidole wakati wa utoto wako? Ulikuwa hukosei ila hukujua faida zake.


MawasilianoMato Eric IT Professional/Digital Marketing Specialist/Digital Content Writer Tel: +255 713 999527 eric.mato9@gmail.com

Related Posts

Post a Comment