Mwanamume mmoja katika jimbo lililo mashariki mwa India, amejenga barabara ya umbali wa kilomita 8 akitumia sururu ili kuwawezesha watoto wake kupitia wakitoka shuleni.
Jalandhar Nayak, 45, anaishi umbali wa kilomita 10 kutoka shule ambapo watoto wake watatu wa kiume husoma.
Lakini safari hiyo huchukua saa tatu kwa sababu vijana hao hulazimika kupitia milima mitano kabla ya kufika nyumbani.
Maafisa wa eneo hilo waliiambia BBC kuwa watamalizia kilomita zingine saba zilizosalia.
Kwa miaka miwili iliyopita aliamka kila asubuhi na vifaa vyake na angetumia hadi saa nane kwa siku kuchimba mawe na kuyaondoa.
Aliwaambia waandishi wa habari kuwa alitarajia wanawe kwenda nyumbani hasa wikendi na wakati wa likizo mara kwa mara baada ya barabara hiyo kukamilika.Barabara hiyo wa kilomita 15 itaunganisha kijiji cha cha Bw. Nayak na mji ambapo shule ipo.
Maafisa wa serikali ambao sasa wamendelea na ujenzi huo walisema kuwa Bw. Nayak pia atalipwa kwa kazi aliyoifanya.
Bw Nayak alisema alikuwa na furaha sana kuwa serikali sasa inaikamilisha barabara hiyo. Pia alisema kuwa aliwaomba kupeleka umeme na maji ya kunywa katika kijiji hicho.
Post a Comment
Post a Comment