Tangazo la
muda mrefu la kufanyika kwa utalii katika hifadhi ya wanyama pori ya ruaha kwa
hisani ya Mgobasa Studios limefanyika kama ilivyopangwa tarehe 8-9 mwezi wa 12/
2017
Tangazo hilo
ambalo limekuwa likitangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari vilivyko mkoa
wa njombe na Iringa liliwataka wapigapicha anaosafisha picha katika studio za
mgobasa zilizoko wilaya ya mbarali Mbeya,njombe,makambako na songea mkoani
ruvuma kushindania kinyanganyiro cha kupata fursa ya kufanya utalii wa ndani.
Mapema saa
kumi na mbili asubuhi siku ya ijumaa nje ya ofisi ya Mgobasa makambako ya kusafisha picha wapigapicha Zaidi
ya 40 wanaanza safari kuelekea ruaha national park kilomita Zaidi ya 85 kutoka kitovu
cha mji wa Iringa.
Baada ya
kuwasili getini kwanza ni kujiandikisha na kisha kupewa maelekezo kupitia maafisa
utalii [tour guides]
Baada ya
mwendo kidogo kila mmoja anahuzunika kuona Wanyama wanaoisi majini wakiwemomaba
na viboko kuishi katika maji yenyekina kifupi na kuonekana wakiteseka,ambapo
waliowengi wanahoji maafisa utalii ni kwaninini maji yamepungua na namna ya
kutatua tatizo,licha ya majibu kutopatikana kwa haraka.
Aidha katika
ziara hiyo ya utalii iliyojumuisha wapiga picha kutoka njombe mjini ,
makambako,rujewa,na songea pamoja na waandishi wa habari itv,clouds media na
kings fm radio,afisa utamaduni makambako na walimu wawili wa shule za msingi
makambako zilizofanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba mjini makambako ambazo
sigridi na azimio,
Imewafanya washiriki
kufanikiwa kuwaona Wanyama kama twiga,tembo,swala,kiboko,mamba,kanga,simba,na
pundamilia kwa siku ya kwanza na kuwafanya kufurahi saana.
Post a Comment
Post a Comment