Dalili hizi zitakupa kujihadhari mapema mara utakapoziona zinajitokeza mara kwa mara katika mahusiano yenu.
Kusudi la makala hii ni kuwasadia wale wenyematarajio yakuingia katika mahusiano ya kushi pamoja kwa sababu wengi wamekuwa vipofu katika kuona baadhi ya dalili mbaya zinazoonekana katika hatua za mwanzoni katika mahusiano na mara wanapoendelea mbele na kufanya maamuzi mazito hususani maamuzi ya kuamua kuoana au kuishi pamoja, mabadiliko makubwa yanaanza kutokea na hali inaanza kuleta misuguano mingi na maumivu mengi baina ya wapenzi, na mbaya zaidi wengine hushindwa kabisa kuendelea na mahusiano nahivyo kuamua kulivunja penzi lao.
Yatupasa wote tuliopo katika mahusiano, kabla ya kuendelea na kufanya maamuzi fulani tuwe tunatazama pia dalili za hatari.
Kwa upande mkubwa dalili hizi zimeegemea kuwasaidia zaidi jinsia ya kike kujua au kuwafahamu wanaume.
Hii ni kwa sababu wanawake ndio ambao wamekuwa wakioyesha kuumizwa zaidi na kukatishwa tamaa na mabadiliko ya tabia za wanaume mara wanapozama katika dimbwi la mapenzi. Ingawa pia wapo pia wanaume wanaoumizwa kutokana na mabadiliko ya tabia za wapenzi wao, nawao pia waweze kuzitazama dalili hizi.
Dalili:
Mpenzi wako anakuwa na wivu sana kwa ule muda unaotumia kuwa na wafanyakazi wenzako, marafiki na hata ndugu zako, ingawa sio kwamba anataka muda huo awe na wewe.
Anakuwa na tabia za kukuudhi na kukutawala, ataangalia sana kutoka na kuingia kwako, nyendo zako na hata matumizi yako ya fedha, na kama ukimuuliza kwanini anafanya hivyo, atajiteteta kuwa anakusaidia kufanya maamuzi sahihi.
Taratibu anakutenga na wote waliokaribu na wewe. Pia anajaribu kukutenga na wale wanaoonekana kuwa msaada kwako kama vile, wale unaowisiliana nao kwa simu, wafanyakazi wenzako na hata ndugu zako wa karibu.
Huwa na tabia ya kuwalaumu sana wengine kwa matatizo anayoyapata. Mfano anapokosa kazi, anaposhindwa shuleni nk. Kila kitu ni kosa la mtumwingine na sio yeye.
Hukasirishwa na kuudhiwa na vitu vidogo vidogo na vyakawaida katika maisha ya kila siku, mfano akiambiwa afanye kazi zaidi ya muda wa ofisi, akiombwa amwangalie mtoto, anapopingwa katika kitu kidogo nk.
Anakuwa na tabia za kikatili kwa wanyama (wafugwao) na hata kwa watoto. Haumizwi pale anapoona maumivu au kuteseka kwa wanyama au watoto.
Anaweza kujiona anacheza au kutania bila kujua anaumiza mtoto au mnyama.
Ni wenyetabia ya mabavu hususani katika tendo la ndoa, hawatojali hisia zako, umelala usingizini au unaumwa, bali hujali zaidi kuzitimiza haja zao.
Ni wenye maneno makali yakuumiza, na ya kushusha hadhi, huweza kukuamsha usingizini ili akutukane au kukugombeza. Akianza malumbano hakupi upenyo wa kwenda kulala, anaweza kulalama usiku mzima.
Sio watu wakutabirika, ni watu wenye hisia za kubadilika badilika, mara muda huu anafuraha na kuonyesha mapenzi, mara ghafla kakasirika na kutaka kuadhibu mtu.
Anaweza akawa na historia ya tabia za kikorofi na kigomvi, labda amewahi kuwa na matukio ya kuwapiga marafiki zake, akijitetea kuwa alipitiwa tu na hasira.
Ni mwenye vitisho na tabia za kuashiria fujo, mfano kupenda kutishia akisema “Nitakuzaba vibao” “Nitakuuwa”, “Nitakuvunja Shingo” “ntakufanyia kitumbaya” n.k.
Mwenyetabia ya kupiga au kugonga vitu kwa hasira, kuvunja vitu vyako, kukurushia vitu wewe au watoto kwa hasira.
Hutumia nguvu anaposisitiza hoja yake, mfano, kukushika nguo au kukukandamiza ukutani na mara nyingine kukusukuma.
Post a Comment
Post a Comment