'Titanic is sinking' Ilikuwa ni title ya kitabu tulichosoma form one mwishoni mwa miaka ya 80...hadithi ya kweli yenye mafunzo mengi baadae ilikuja kutengenezwa sinema iliyojivunia umaarufu mkubwa duniani, sinema ya TITANIC ndani ya ile sinema iliyobeba hisia nyingi za mapenzi usaliti ubabe na dharau kuna mafunzo na darasa kubwa tuliloachiwa
√KUKOSA UMAKINI
Nahodha mahiri akiwa anaongoza meli kubwa duniani isiyozama, ananasa tukio la DiCaprio na mpenzi wake wakiwa kwenye pozi la mahaba mazito.. Badala ya kuangalia kazi yako anajisahau kabisa na kukodoa macho ya utamanifu
√DHARAU
Nahodha kuja kushtuka naona kitu Kama Kichuguu cha barafu lakini anadharau akidhani kile ni Kichuguu kidogo na si mwamba mkubwa...kwakuwa tu TITANIC IS UNSINKABLE...!!!
√USALITI
yule binti baada ya kulazimishwa kuolewa na tajiri mwenye kila kitu alikuja kusaliti ndoa yake kwa kijana mdogo kapuku
√UBABE NA PESA SI KILA KITU MAISHANI
tajiri yule aliamini kuwa kwa pesa yake angeweza kupendwa na yoyote.... Lakini matokeo tuliyaona. Mapenzi ya kweli hayachagui
√UPWEKE NA KUHUKUMIWA NA ROHO
yule binti alikuja kuishi mpweke Mpaka anakufa miaka michache iliyopita..true love happens once in the life time
Kuna mengi yaliyo hai ya kujifunza hata katika maisha yetu ya leo hii.... Yaliyojiri wiki nzima iliyopita na hitimisho lake pale ubungo leo havitofautiani sana na habari ya Titanic
Tuliokuwa tunadhani kile ni kisiki tulikosea sana.... Kumbe ule ni mwamba mkubwa na kwa dharau zetu na kiburi kilichopitiliza our TITANIC IS SINKING... =======
Post a Comment
Post a Comment