
Baba mmoja katika mji wa Coimbatore nchini India ameiteketeza familia yake kwa kuichoma moto akikwepa kulipa deni la Shilingi 4,300/= za kitanzania. Miili mitatu ya familia iliyoungua kwa moto ikipelekwa hospitali mapema jumatatu baada ya kutokea kwa tukio hilo Mwanamme huyo aliyetambulika kwa jina la Esakimuthu alifanya tukio hilo siku ya jumatatu tarehe 23 Otoba ambapo aliwamwangia mafuta ya taa mke wake aliyetambulika kwa jina la Subbulakshmi na watoto wake wawili wakiwa wamelala na kuwachoma moto kisha na yeye kujiua .

Taarifa za uchunguzi kutoka polisi zinasema mdaiwa huyo kabla ya kuchoma moto familia yake kuna mtu alikuja nyumbani kwake siku moja kabla ya tukio akimdai kiasi cha rupia 96 kama ongezeko baada ya kumkopesha rupia 1 miezi mitatu iliyopita. Polisi wamekiri kuwa mdaiwa wiki iliyopita alitoa taarifa kwao kutaka suala la kudaiwa lisuluhishwe, hata hivyo polisi walimtaka alipe kiasi hicho kama walivyokubaliana ndipo mdaiwa akachukua uamuzi huo. Chanzo:The Hindu
Post a Comment
Post a Comment