Ikiwa ni miezi 11 tangu Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ahamie Makao Makuu ya Tanzania, Dodoma, viwanja zaidi ya 22,000 na hoteli za kifahari katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma vinatarajiwa kuondolewa ili kupisha makazi ya ofisi yake.
Mkurugenzi wa Manispaa Dodoma, Godwin Kunambi akizungumzia suala hilo alisema kuwa, “Tumewajulisha wamiliki wasitishe kufanya muendelezo kwa majengo ya hoteli hizo kwa kuwa zipo karibu sana na makazi ya Waziri Mkuu na hatuwezi kuruhusu hoteli hizo ziendelee kuwa hapo kwa sababu za kiusalama.”
Alisema ubomoaji huo pia ni njia ya kuendelea kuupanga mji huo ambao sasa unakaliwa na viongozi wengi wa serikali na kwamba kadiri siku zinavyozidi kwenda wataongezeka wengine.
Akitaja hoteli zilizopo karibu na makazi hayo mbazo zitabomolewa, Kunambi alisema hoteli hizo ni pamoja na African Dream, Royal na nyingine mpya.
Walipotafutwa kwa ajili ya maoni yao wamiliki wa hoteli walisema kuwa bado hawajapewa taarifa rasmi lakini alisema wapo tayari kuondoka na kubomoa majengo hayo iwapo watapata fidia stahiki kwa mali zao.
Kunambi alitoa nafasi ya mwezi mmoja watu waliopewa barua za viwanja wawe wamekamilisha kuvilipia kabla ya maeneo hayo kutwaliwa.
Hapa chini ni baadhi ya picha za Hoteli ya African Dream iliyopo Dodoma.
Post a Comment
Post a Comment