Jioni ya jana, mwanadada maarufu ambaye anatumiwa na wanamuziki nchini kupendezesha video za nyimbo zao ambaye pia ni msanii wa muziki wa Bongofleva, Amber Lulu jana alifikishwa kwenye kituo cha polisi Urafiki jijini Dar es salaam kutoa maelezo ya uhusika wake na usambazaji wa picha alizopiga akiwa mtupu pamoja na mwanamuziki mwenzie, Young Dar es salaam (Young D).
Amber Lulu alihojiwa kwenye kituo hicho na kuachiwa saa chache baadaye baada ya kukamilisha kutoa maelezo aliyotakiwa.
Juhudi za kumtafuta Aber kwa ajili ya kutoa taarifa ya tukio hili zimegonga mwamba kwakuwa simu yake haipokewi kwa muda wote tuliompigia.
Tukio hili la kuhojiwa na polisi limetokea baada kusambaa kwa picha iliyozua gumzo kubwa la kimaadili inayomwonesha Amber akiwa ameziba matiti kwa kutumia mikono tu akiwa amevaa nguo ya ndani aina ya bikini pekee huku Mwanamuziki Young D akikodolea macho makalio ya mwanadada huyo.
Post a Comment
Post a Comment