Bado masaa yasiyozidi 40 ili dirisha la usajili barani Ulaya kufungwa, kila timu inajaribu kupata sahihi ya mtu sahihi kwa ajili ya msimu huu wa ligi na matumizi makubwa ya pesa yanafanya muda huu uliobaki kuwa wa kuvutia.
Thomas Lemar ambaye alikuwa anatajwa kuelekea Anfield kukipiga na klabu ya Liverpool inaonekana Barca wameingilia kati usajili huo na sasa wanataka kumnunua Lemar, taarifa zinadai Barca wanapambana kuipiku Liverpool ndani ya usiku wa leo au kesho.
Oxlade Chamberlain naye amekuwa akizungumziwa sana hii leo, Chamberlain alikuwa akihusishwa kuelekea Stamford Bridge na inasemekana Chelsea walishakubali kutoa £35m ili kumnunua lakini leo habari mpya zinadai Chamberlain amekataa kujiunga na Chelsea na anataka aende Liverpool.
Angel Di Maria anaweza kurudi tena katika ligi kuu ya Hispania La Liga, lakini kubwa zaidi ni kwamba safari hii Di Maria anarudi Hispania ambako anatakwa na wapinzani wakubwa wa timu yake ya zamani Real Madrid ambao ni Barcelona, taarifa zinasema Di Maria amemuomba kocha Unai Emery kumruhusu aende Hispania.
Inaonekana pamoja na matatizo yote yaliyotokea kipindi hiki cha usajili lakini Ross Barkley anabaki Everton, klabu hiyo imeitolea nje Chelsea ambao walionesha nia ya kumtaka lakini Everton wameikataa ofa yao ya £25m.
Jose Mourinho baada ya kumkosa Ivan Perisic anaonekana kuvutiwa na kumnunua Ryad Mahrez toka Leicester City, lakini mabosi wa Manchester United hawapendezwi na usajili wa Mahrez na hawako tayari kutoa kiasi cha pesa kwa Mualgeria huyo.
Post a Comment
Post a Comment