Hayo yamesemwa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi wakati akiwasilisha hoja na kujibu maswali mbali mbali kwenye Kamati nne za kudumu za bunge kuhusu miswada mitatu inayohusu raslimali za Taifa.
Prof. Kabudi amesema Serikali sio naive na inafahamu dunia ilivyo kuhusu economic order. Tunajua we are fighting giants but we cannot be afraid of giants. Tunatumia akili nyingi, hekima na busara katika vita hii.
Aliendelea kusema, ‘’We know there will be an attempt to sabotage, definitely na kama tuki-succumb kwamba we are fight a giant busi tukae, tutakuwa hatulitendei haki Taifa’’.
‘’This country has survived sabotage, miaka mingi tu, na sisi lazima tujaribu kuliko kukaa chini na ku-succumb’’ alisema.
Aliendelea kusema‘’Hatuwezi kuwa na wawekezaji ambao hatufaidiki nao nani bora madini tuyaache badala ya kuyachimba ili tusubiri hao kizazi kijacho watakaokuwa na busara na akili kwa sababu sisi tumeshindwa. Madini huwa hayaozi’’
‘’Sheria hii tutakayotunga haiwafukuzi bali inawakaribisha kwa mazungumzo, waje tuongee, tutaelewana na uzuri mambo tunayoyadai yamo ndani ya sheria za kimataifa, hatuyazui wenyewe. Mikataba ya sasa itaangaliwa, tutajadiliana nao. Hatufukuzi mtu na hawawezi kufunga migodi kwa sababu tunafahamu wanapata faida’’.
‘’Yes, we fighting giant, biashara ya dhahabu inafahamika nani ana control lakini huyo giant unapomfikisha anarusha ndege kuja nchini kujadiliana, hayo ni mafanikio’’
‘’Kama Botswana yenye wananchi milioni 2 inaweza ku-flex its muscles kwenye maliasili zake, sisi Watanzania ambao ni 50 millions, we are lame ducks and toothless bulldog. It's incredible’’.
‘’Tusisahau kuwa nchi hii ime survive kwa vitisho vikubwa kuliko leo. Mwaka 1964, Mwalimu angetetereka kwa Wajerumani waliokuwa wanatupa hela nyingi, akawasikiliza, Tanzania isingekuwepo kama Jamhuri ya Muungano. Kwa msimamo wa Mwalimu, tulipoteza Deutsche Mark milioni 35 lakini Mwalimu akawaambia pack and go’’.
‘’Mwaka uliofuata, 1965 kulitokea Unilateral Declaration of Independence (UDI) in Rhodesia ambapo nchi zote za Afrika zilikubaliana lazima Uingereza imuondoe Prime Minister, Ian Smith ama sivyo nchi zote zitavunja uhusiano wa kibalozi na Uingereza. Baada ya Uingereza kukataa, nchi mbili za Tanzania na Ghana ndizo zilivunja uhusiano wa kibalozi ambapo gharama yake ilisababisha Rais wa Ghana kupinduliwa huku Tanzania tukikosa msaada wa pound milioni 5’’.
‘’Malengo ya mifano yangu sio kwamba turudie hayo bali kuonyesha kuwa Taifa hili limepita vipindi vigumu kwa sababu lilikuwa na uongozi unaothubutu na kusimamia maslahi ya watu ili liweze kuvuka. Hiki ni kipindi kingine cha kuvuka’’.
‘’Tusiogope na kuanza kuulizana kuwa tutaweza au hatutaweza? Wawekezaji watatishia kuwa wataondoka lakini ninasema hawataondoka’’.
Prof. Kabudi amesema watu wa ACACIA kinachowasumbua siyo sheria bali ni integrity yao kwa sababu kampuni inayovunja integrity pledge hupelekea kushitakiwa kwa kosa la fraud. kampuni inayofanya fraud na ikadhibitika kisheria, mali zake hutaifishwa. Hiki kinafanyika hata kwenye nchi zao za Ulaya na Marekani’’.
Alisema, ‘’Ukiona ACACIA wanavyohangaika ambapo mara ya kwanza waliomba kuonana na Rais ambaye maombi yao aliyakataa. Wakaomba tena mara ya pili na kukubaliwa kupitia Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambaye ni mmiliki mkubwa wa hisa 63.9 wa Kampuni ya Acacia Mining, Profesa John Thorton’’.
‘’Kwao integrity ni muhimu sana kutokana na heshima ya kampuni ambayo wajumbe wa bodi ni viongozi wastaafu wenye heshima kubwa duniani’’.
Alimaliza kwa kusema, Watanzania tunatakiwa tujiamini kwa sababu nchi yetu ime train watu wengi katika fani mbali mbali pamoja na fani ya madini lakini tatizo lililopo ni kutowathamini, kuwadharau na kutowatambua. Hatukuwatumia na wameondoka kwenda kusaidia nchi nyingine. Kwa mfano, Nchi ya jirani tunayoisifu kuwa miji yake imepangwa vizuri, wataalam waliochora ramani ya miji hiyo wametoka Tanzania. Director of finance wa Air Tanzania ndio alikuwa Director of finance wa Air Rwanda. Ndiye ameiwezesha Air Rwanda kufika hapo ilipo. Key staff wa Air Rwanda ni Watanzania ambao baadhi yao wamekubali kurudi. Tatizo letu watanzania tunajidharau wenyewe wakati uwezo tunao’’.
Kwa maelezo zaidi angalia video.
Post a Comment
Post a Comment