const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); MAMLAKA YA ANGA (TCAA) YAZUIA MATUMIZI YA DRONES - HABARI MPYA

..

MAMLAKA YA ANGA (TCAA) YAZUIA MATUMIZI YA DRONES


Serikali kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imezuia matumizi ya ndege zisizo na rubani maarufu kama drones katika anga la Tanzania bila kuwa na kibali cha mamlaka husika.

Katika tangazo lililotolewa na mamlaka hiyo kwa vyombo vya habari imesema kuwa, uendeshaji wa ndege zote katika anga la Tanzania unatakiwa kuidhinishwa au kupata kibali kutoka TCAA.

Kufuatia hayo, TCAA imesema kuwa, taasisi, kampuni au mtu yeyote anayetaka kuendesha, kujaribu ndege hizo zisizo na rubani, ni lazima apate kibali cha Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, na pili ni idhini kutoka TCAA.

Hapa chini ni tangazo la TCAA kuhusu matumizi ya ndege hizo.

ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!


Related Posts

Post a Comment