PWANI: Dunia imekwisha! Fadhil Mshamu, mkazi wa Kibaha Kwa Mfipa mkoani Pwani, Jumanne iliyopita alikumbwa na aibu kubwa, baada ya kubambwa na polisi, akidaiwa kumshawishi binti yake wa kumzaa ili ampe penzi.
…Baba huyo akiwa na mwanaye aliyekuwa akimfosi penzi.
UANZE MKASA HUU KWA UMAKINI
K i t e n g o Maalum cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers, mwanzoni mwa wiki hii kilipokea simu kutoka kwa mwanamke mmoja, aliyedai wanahitaji msaada kwani katika familia yao, kuna tatizo kubwa ambalo limewasumbua kwa muda mrefu.
… Akiwa katatiwa na polisi.
M w a n amke huyo a l i y e d a i a n a i s h i Buguruni jijini Dar es Salaam, alipotakiwa k u d o k e z a tatizo hilo, alidai kuwa katika familia yao, kuna baba anataka kuvunja amri ya sita na binti yake!
OFM WASHTUKA, WATUA BUGURUNI
Kwa taarifa hiyo ya kushtusha, makamanda wa OFM walilazimika kufika Buguruni ili kupata habari kamili na kufika huko, walikutana na mwanamke aitwaye Tatu Mshamu waliyezungumza naye kwa simu, ambaye alijitambulisha kama shangazi wa binti anayetakiwa kutenda dhambi hiyo na baba yake!
HUYU HAPA SHANGAZI
“Huyu ni mtoto wa kaka yangu, kila siku anatuambia baba yake anamsumbua, anamtaka kimapenzi. Tumejaribu kukaa naye na kuzungumza, lakini anatuambia watoto wanamsingizia tu, siyo kweli. Tunajiuliza kwa nini kila siku wakusingizie wewe tu?
“Sasa leo tukaona labda kweli hawa watoto huenda wana lao jambo, tukamwambia huyu binti, hebu tuthibitishie kama unachoongea ni cha kweli, akasema ngoja apige simu kwa baba yake, akaweka laudi spika!
“Akampigia mbele yetu, tukawa tunamsikia anavyombembeleza. Sasa sisi tumechoka, tunataka hili jambo bora lijulikane, maana tumezungumza naye haelewi, kama mbwai na iwe mbwai tu!”
FAMILIA YAJIPANGA KUMNASA BABA
Wanafamilia hao waliwaambia makamanda wa OFM kuwa walikuwa wameandaa mtego wa kumkamata baba huyo, kwani tayari alishaanza mawasiliano na mwanaye, akimtaka kwenda Kibaha Kongowe ili kwenda kujivinjari naye.
Baada ya kusikia madai hayo mazito na jinsi ya kukutana eneo la tukio, makamanda wetu wakitumia usafiri wao wa mwendokasi, waliwasili Kibaha Kongowe salama salimini kabla ya kupokea simu kutoka kwa shangazi mtu, akiwaelekeza jina la gesti ambayo baba mzazi alikuwa akimsubiri binti yake.
NEW KILAWENI GUEST HOUSE
Kwa kuwa makamanda hao walikwishamtambua binti huyo anayedai baba yake kutaka afanye naye ufuska huo, walipofika eneo la tukio, njia ya Soga eneo la Kwa Mmbaga, walimuona akiwa amekaa kwenye kiti na meza ambayo pia alikuwepo mwanaume akinywa bia, ambaye kwa harakaharaka waliamini alikuwa ndiye baba yake mzazi.
POLISI WAIBUKA, K I Z A A Z A A CHAZUKA
OFM wakiwa hawana hili wala lile, ghafla wakaona kundi la askari zaidi ya nane wakiibukia eneo hilo, wakiwa w a m e o n gozana na shangazi wa binti, Tatu Mshamu na mama mzazi wa binti, Antonia Mango.
K i t e n d o cha watu hao kuibuka eneo hilo ghafla, kilimfanya baba mtu kuhamaki, hasa baada ya k u amb iwa kuwa yupo chini ya ulinzi kwa tuhuma ya kufosi penzi kwa binti yake.
ETI WALISHAZAMA GESTI
Katika hali ya kushangaza, binti huyo aliuambia umati uliokusanyika hapo kuwa kabla hawajatokea, baba huyo alimpeleka katika chumba cha gesti hiyo na kutaka walale lakini akamkimbia.
“Alinipeleka chumba namba moja, kulikuwa na kitanda tu, akawa anataka tulale, mimi nikakataa, akanifichia viatu vyangu, nikamponyoka nikaja hapa, ndiyo akanifuata akawa ananibembeleza,” alidai binti huyo na kuwaacha watu midomo wazi.
MHUDUMU WA GESTI ASIMULIA
Mhudumu wa gesti hiyo ambaye jina lake halikupatikana mara moja, aliwathibitishia polisi kuwa baba huyo alikodi chumba na kuingia na binti huyo chumbani.
AKUTWA NA FUNGUO, ATAITIWA
Huku akiendelea kubisha kuwa hakuingia na binti yake chumbani, mzee huyo alikutwa na ufunguo wa chumba namba moja wa gesti hiyo, kitu kilichosababisha akose la kusema.
Polisi walimtaiti na kumtaka waelekee chumba walichoingia, ambacho kilikuwa na kitanda tu na kulazimishwa kuonyesha alikoweka viatu vya bintiye, ambavyo baadaye vilikutwa vikiwa katika kona ya chumba hicho.
SHANGAZI, MAMA
WAZUA TIMBWILI
Kuona hivyo, shangazi na mama mzazi wa binti huyo ambaye kwa sasa alishaachana na mwanaume huyo, walianza kumshambulia, wakimtuhumu kuwa anafanya mambo ya aibu.
Timbwili hilo lililoambatana na maneno mazito kutoka kwa mama na shangazi huku baba mtu akijibu mashambulizi, lilichukua muda mrefu kabla ya mtuhumiwa kugeuka ‘mdogo kama piritoni’ kwa aibu.
WASOMBWA POLISI
Kufuatia sakata hilo, maafande hao waliwachukua mama, shangazi, binti huyo na baba yake na kuwapeleka Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kibaha ambapo baada ya mahojiano walimfungulia jadala la uchunguzi lenye namba KBA/ RB/4067/2017.
Baadaye baba huyo alihamishiwa Kituo Kikuu cha Mkoa na kufunguliwa jalada lingine lenye namba KBA/ IR/2278/2017 JALADA LA UCHUNGUZI.
Mpaka gazeti hili linakwenda mtamboni haikufahamika kilichoendelea baada ya hapo ila tunaahidi kuwaletea muendelezo wa habari hii kwenye magazeti yanayofuata ya Global Publishers.
chanzo: GPL
Post a Comment
Post a Comment