const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); RASMI IBRAHIM AJIBU NI MALI YA YANGA - HABARI MPYA

..

RASMI IBRAHIM AJIBU NI MALI YA YANGA

Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu imefahamika kuwa sasa ni rasmi anajiunga na Yanga baada ya klabu yake ya sasa kushindwa kufikia nae makubaliano ya kumbakiza kwenye kikosi.
Mabosi wa Simba na mchezaji huyo wameshindwa kuafikiana juu ya makubaliano ya mkataba wake mpya na hiyo imewapa nafasi Yanga waweze kumchukua.

Taarifa kutoka ndani ya Simba imeeleza kuwa wameamua kumruhusu aondoke baada ya mchezaji huyo kuonyesha kutokuwa na nia ya kuendelea kubaki klabuni hapo.

“Tumemwacha aende anakotaka kwenda kwa sababu hana ‘spirit’ tunayoihitaji sisi, acha aende tu sisi mbele kwa mbele,” amesema mtoa taarifa.

Ajib ambaye alianza kutamba Simba akitokea kikosi cha vijana, atatua Yanga aliwa mchezaji huyu kutokana na mkataba wake kuelekea mwishoni.

 ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!


Related Posts

Post a Comment