Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Elisha Mghwira leo ametembelea familia ya marehemu Mzee Philemon Ndesamburo na kutoa pole kwa ndugu na jamaa waliokuwa nyumbani kuomboleza msiba wa mpendwa huyo.
Anna Mghwira aliyeapishwa juzi Ikulu jijini Dar es Salaam ameanza kazi rasmi leo katika kituo chake cha kazi ambapo alikwenda nyumbani kwa aliyekuwa Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo na kupata nafasi ya kuzungumza na mke wake na kumpa salamu za pole kufuatia kufiwa na mumewe.
Mzee Ndesamburo alifariki wiki iliyopita muda mfupi baada ya kupata matatizo ya kiafya akiwa ofisini kwake na alizikwa siku ya Jumanne nyumbani kwake Kiboroloni Moshi Mjini.
Post a Comment
Post a Comment