Kampuni ya Acacia imeipinga ropoti ya pili ya uchunguzi wa Makinikia iliyowasilishwa kwa Rais Dkt Magufuli na kamati iliyokuwa chini ya Prof. Osoro ambayo imeituhumu kampuni hiyo kufanya madanganyo katika biashara yake.
Ripoti hiyo iliyowasilishwa leo Ikulu mbele ya viongozi mbalimbali ilieleza kuwa, Acacia wamekuwa wakidanganya kuhusu mapato yao na kodi wanayotakiwa kulipa kutokana na biashara ya uchimbaji wa madini.
Kamati hiyo ilisema kuwa Acacia sio wanaosafirisha makinikia hayo kwenda nje ya nchi bali huziuzia kampuni za Ujerumani, Japan yakiwa bado yako hapa nchini lakini wao huidanganya serikali kwamba wanasafirisha yakachenjuliwe ndipo wajue gawio ambalo serikali itapata.
Acacia wamesema kuwa rupoti hiyo haiendani na hali halisi ya utendaji kazi wao nchini kwa miaka 20 na kwamba ripoti hiyo imekuza mambo ambayo si ya kweli.
Miongoni mwa mapendekezo ya kamati hiyo ni pamoja kampuni hiyo kulipa malimbikizo ya tozo zote tangu mwaka 1998 ndipo Tanzania ikubali kukaa na kujadiliana nao kuhusu usajili na pia kupitia upya mkataba wa kazi.
Hapa chini ni taarifa ya kampuni hiyo;
Post a Comment
Post a Comment