Soka ni pesa, zamani ilikuwa washambuliaji tu wanaonunuliwa kwa gharama kubwa lakini sasa hadi magolikipa bora ni ghali na ndio maana haishangazi United kukataa euro 66m kwa ajili ya David De Gea, hawa hapa ndio walinda milango ghali duniani kwa sasa.
10.Fraser Foster na Asmir Begovic. Foster ni golikipa wa klabu ya Southampton ambaye alisajiliwa kutoka katika klabu ya Celtic mwaka 2014, pesa iliyotumika kumnunua Fraser Foster haikuwa ndogo kwani Southampton walitumia euro 10m kumnunua lakini Chelsea nao wakatumia kiasi hicho cha pesa kumnunua Asmir Begovic kutoka Bournamouth.
9.Petr Cech. Mlinzi mkongwe ambaye alikuwa na kiwango bora sana alipokuwa Chelsea na ni lazima kumtoa katika klabu ya Chelsea kulihitaji kiasi kikubwa cha fedha na Arsene Wenger alitoa euro 10.9 kumnunua mwaka 2015.
8.Jan Oblak. Msimu huu yupo katika kikosi bora cha ligi ya Champions League na tayari vilabu vingi vinamtamani na klabu ya Atletico Madrid ilitumia kiasi cha euro 12.6m kutoka Benfica mwaka 2014.
7.Jasper Cillessen. Mwaka 2016 klabu ya Barcelona walimuona Cillessen kama mlinda lango bora, Cillessen alikuwa akiidakia Ajax ya nchini Uholanzi na klabu ya Barcelona iliamua kutoa kiasi cha euro 12.8m.
6.Angelo Peruzzi. Golikipa wa Lazio ambaye alinunuliwa mwaka 2000 kutoka katika klabu ya Inter Milan, Lazio walitoa kiasi cha euro 15.7m kumnunua Angelo Peruzzi ambapo akawa mlinda lango ghali katika klabu ya Lazio.
5.Claudio Bravo. Pamoja na kelele nyingi kuhusu makosa anayoyafanya Claudio Bravo lakini Manchester City walitumia kiasi kikubwa sana kumnunua kutoka Barcelona ambapo kiasi cha euro 17m kumnunua Bravo.
4.David De Gea. Labda kwa sababu Manchester United walitumia kiasi kikubwa cha fedha kumnunua De Gea mwaka 2011 kutoka Atletico Madrid ndio sababu wanataka kiasi kikubwa kutoka Real Madrid, United walimnunua De Gea kwa euro 18m.
3.Manuel Neuer. Kati ya magolikipa ambao kuna nyakati alitajwa kwamba anafaa kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa dunia, Manuel Neuer alinunuliwa na Bayern Munich kutoka Schalke 04 mwaka 2011 kwa dau la euro 19m.
2.Gianluigi Buffon. Golikpa ambaye pamoja na ubora wake wote lakini ameshindwa kuchukua kombe la Champions League, Buffon alinunuliwa na Juventus kutoka Parma mwaka 2011 kwa dau la euro 33m.
1.Ederson. Usajili huu umekamilika rasmi leo ambapo Emerson amesaini mkataba wa miaka mitano kuitumikia klabu ya Manchester City, Emerson amenunuliwa kwa dau la euro 34m kutoka Benfica na anakuwa golikipa ghali zaidi duniani.
Post a Comment
Post a Comment