Baada ya habari kubwa iliyotoka leo kuhusu Diego Costa kuambiwa na kocha wake Antonio Conte kwamba hahitajiki msimu ujao wa ligi tayari vilabu mbalimbali vimeshaanza kupiga hodi katika klabu ya Chelsea huku Ac Millan wakitajwa kuwepo mstari wa mbele kumnunua Costa.
Manchester City wamethibitisha kumnunua mlinda mlango wa Benfica Ederson Moraes kwa dau la euro 35m, Moares mwenye umri wa miaka 23 amesaini mkataba wa miaka mitano kukipiga katika klabu ya Man City.
Pamoja na klabu ya Liverpool kuiomba msahamaha Southampton kuhusu suala la kutaka kujaribu kumsaini mlinzi Virgil Van Dijk bila kuwasiliana nao, klabu ya Southampton bado imesisitiza kwamba Liverpool lazima wafikishwe mbele ya sheria na kuchukuliwa hatua.
Klabu ya Real Madrid imewaambia Monaco kwamba Kylian Mbape hana thamani ya zaidi ya euro 100m kama wanavyodai, na Real Madrid wanasema pesa kubwa ambayo wanaweza kutoa kumsaini Mbappe ni euro 85m.
Juanma Lopez ambaye ni wakala wa Alvaro Morata amesema mteja wake hana uhakika kucheza Real Madrid msimu ujao kwani anahitaji muda mwingi wa kucheza tofauti na ule anaopewa na Real Madrid na hii inaweza kuwa habari njema sana kwa Manchester United.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!
Post a Comment
Post a Comment