Kylian Mbappe anatajwa kuwa na thamani ya zaidi ya euro 100m kiasi ambacho kinaweza kuweka rekodi mpya ya usajili, Mbape ana miaka 19 tu lakini kuna hawa wachezaji watano ambao nao ni hatari hadi sasa na walinunuliwa kwa pesa ndefu wakiwa hawajafikisha miaka 20.
5.Sergio Aguero. Mwaka 2006 alikuwa na umri mdogo tu wa miaka 17 ambapo klabu ya Atletico Madrid walimuona akiichezea klabu ya Independiente na kutokana na uwezo wake mkubwa waliona kiasi cha euro 15m kinatosha kumchukua mshambuliaji huyo.
4.Sergio Ramos. Beki wa kutumainiwa wa klabu ya Real Madrid lakini mwanzo alikuwa akikipiga Sevilla na ilipofika mwaka 2005 Real Madrid walimnunua Ramos kutoka Sevilla kwa dau la euro 18.5m akiwa na umri wa miaka 19 tu na sasa amekuwa mlinzi bora haswa.
3.Wayne Rooney. Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United alinunuliwa akiwa na miaka 18 kutoka katika klabu ya Everton mwaka 2004 na katika michezo 460 ambayo ameichezea klabu ya Manchester United mshambuliaji huyo amefunga jumla ya mabao 198.
4.Gabriel Jesus(19). Ukiongelea kinda ambaye amefanya makubwa ndani ya muda mfupi ni Jesus, huwezi amini kwamba huyu Jesus ndio ambaye mwaka 2014 alikuwa akipaka rangi mitaani nchini Brazil, alinunuliwa kwa euro 27m kutoka Palmeiras na hadi sasa anaonekana bora sana kuendana na thamani yake.
5.Lucas Moura. Kama ilivyo kwa Jesus huyu naye ni Mbrazil ambaye alikuwa akikipiga katika klabu ya Sao Paulo na tangu akiwa hajafikisha miaka 15 vilabu vikubwa duniani vilishaanza kumgombani lakini PSG walifanikiwa kumsaini kwa euro 28m, alikuwa na miaka 19 tu wakati akisajiliwa.
Post a Comment
Post a Comment