Ilikuwa ni tetesi lakini sasa ni ‘DoneDeal’ baada ya klabu ya Simba kumsaini golikipa huyo kutoka klabu ya Azam FC.
Manula amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba kwa dau la shilingi milioni 50 za Tanzania.
Awali kulikuwa na minong’ono kwamba Manula ambaye ni mshindi wa tuzo ya golikipa bora VPL msimu uliopta amesaini kujiunga na Simba lakini klabu ya Azam kupitia kwa afisa habari wao Jafar Idd walikanusha taarifa hiyo na kusisitiza Azam ipo kwenye mazungumzo ya mwisho na Manula ili kumuongeza mkataba.
Manula anakua mchezaji wa pili kujiunga na Simba akitokea Azam baada ya awali John Bocco kuondoka kwenye klabu hiyo na kuelekea Msimbazi akiwa mchezaji huru.
Post a Comment
Post a Comment