Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na watoto, Dkt Hamisi Kigwangalla amesema katika miaka yake 7 ya uwakilishi bungeni hajawahi kushuhudia bajeti ikishangiliwa kama ya Wizara ya Fedha huku akisema bajeti hiyo inaenda kuwagusa watu wengi.
Dkt Kigwangalla ametumia ukurasa wake wa Instagram kuisifia bajeti hiyo.
Katika miaka yangu saba ya uwakilishi #Bungeni sijawahi kushuhudia bajeti ikishangiliwa na wabunge kama ya jana. Kwa hakika bajeti ya 2017/18 inaenda kuwagusa watu wengi, kuanzia wakulima wetu wadogo wadogo hadi wakubwa hadi wenye viwanda vyenye fungamanisho na kilimo; wachimbaji wadogo hadi wakubwa. Kila mtu ameguswa. Dr. Mpango amekuja akiwa amejipanga haswa, kwa niaba ya Serikali yetu nzima. Michango mingi ya Wabunge na Mawaziri ameizingatia sana. Naamini huu usikivu ndiyo sababu ya bajeti kupendwa na kushangiliwa kiasi hicho. Kwa hakika itapita bila shida. Tutabaki na kazi ya kufanya kazi kwa bidii kuitekeleza. #bajeti #Bajeti2017 #HK #HamisiKigwangalla #Dr_Kigwangalla #SiasaNiVitendo
Juzi Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango aliwasilisha bungeni mapendekezo ya makadirio ya bajeti ya serikali kwa mwaka 2017/18.
Post a Comment
Post a Comment