MADIWANI wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa wameishauri halmashauri hiyo kuongeza vyanzo vya mapato ili kuongeza makusanyo yake kutokana na uchumi wa mazao ya misitu kushuka na kuomba uboreshwaji wa Barabara na kupima viwanja.
Ndani ya baraza la madiwani la kawaida la halmashauri hii ya wilaya wanatoa ushauri huo baada ya kubaini kuwa mapato yake yameanza kushuka.
Akitoa taarifa ya fedha mwenyekiti wa kamati hiyo anasema mpaka kufikia mwezi huu imekushanya asilimia 58 ya malengo iliyo jiwekea.
Pamoja na ushauri huo unaotolewa na madiwani inadaiwa kuwa kunawatendaji ambao hawafanya kazi yao ipasavyo kukusanya mapato.
Halmashauri ya wilaya ya Mufindi ni miongoni mwa halmashauri ambazo zinazalisha kwa kiwango kikubwa mazao ya miti kama mbao nguzo na mazao mengine kutokana na misitu ya kupandwa ambayo ndio chanzo chake kikubwa cha mapato.
Post a Comment
Post a Comment