const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Sheikh Ponda amvaa, Kamanda Sirro, Mwigulu - HABARI MPYA

..

Sheikh Ponda amvaa, Kamanda Sirro, Mwigulu

HATUA ya Jeshi la Polisi kumpiga risasi na kumuua Kijana Salum Almasi la aliyeuawa kwa madai ya ujambazi, imemuibua Sheikh Ponda Issa Ponda.

Sheikh Ponda ambaye ni Katibu wa Taasisi za Kiislam Tanzania amemwandikia ujumbe wa maneno waziri wa mambo ya ndani

Ponda amesema kuwa alipata taarifa za kijana jana Salum Almasi kuwawa hadharani kwa kupigwa risasi na Polisi majira ya saa 3:00, na saa 4:00, asubuhi eneo la Kurasini Dar es Salaam akiwa anatembea barabarani kwa miguu.

“Taarifa ya Polisi ni kuwa kijana huyo ni jambzi aliyetaka kupora fedha. Nimekutana na familia ya Marehemu ambaye ni mzaliwa wa Kilwa, familia inamtambua kuwa ni kijana mwema kabisa. Nimeongea na baadhi ya wakazi wa Kilwa, wao pia wanamtambua kama mtu mwema kwa tabia na anayeshiriki ibada Msikitini ipasavyo.” Ameeleza Ponda.

Ponda amesema Salum Mohamedi pia ni Imamu Msaidizi katika moja ya Misikiti Kurasini. Maelezo ya ziada Salum muda mwingi ni mtu wa masomo. Amemaliza Elimu ya Msingi, Kidato cha Nne, cha Tano, Kidato cha Sita na mpaka anauwawa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ngazi ya Diploma fani ya Tehema (ICT).

Mheshimiwa Waziri Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani, nakusalimu sana. Pia nakutakia ufanisi katika kulitumikia Taifa. Baada ya hayo ninayo haya ya kusema. Katika baadhi ya hafla nilizohutubia hivi karibuni, nilitumia fursa hiyo kueleza masikitiko yangu kwa mauwaji ya askari Polisi zaidi ya watano waliouliwa na watu wasiojulikana hivi karibuni Mkoani Pwani. Natumia fursea hii pia kwako kutamka hivyo. Aidha

Hata hivyo Shekh Ponda akielekeza ujumbe kwa Waziri Nchemba amesema mauwaji kama haya yanazidi kupambamoto Tanzania na yanachafua haiba ya Taifa. Gazeti la Mwananchi la Mei 6, 2017, lilikuwa na kichwa cha habari kisemacho "WALIOUWAWA RUFIJI WAFIKIA 29". “Wananchi wanaouliwa ndugu zao au jamii kwa ujumla wanapoteza haki ya kujuwa ndugu au rai wenzao ni wahalifu kweli au wanauwawa kwa sababu nyingine”.

“Sisi tumeshuhudia ulivyo tufikisha katika Taifa (Tanzania), lenye utulivu na mahusiano mazuri kati ya Jamii na vyombo vya Dola. Vilevile umetufikisha katika Taifa la kistaarabu lisilofurahishwa na umwagaji wa damu kiholela. Ni vizuri Serikali ikatowa tamko la kufafanuwa sababu inayopelekea watu wengi kiasi hicho kuuwawa bila ya kufikishwa Mahakamani.

Related Posts

Post a Comment