Vifuatavyo ni vyakula vinavyoweza kusaidia kuimarisha afya ya ngozi:-
Asali ambayo hutengenezwa na nyuki huwa na viambato asilia na ni moja ya chakula muhimu kwa ajili ya kuimarisha afya ya ngozi . Asali husaidia kutunza na kuhifadhi unyevu kwenye ngozi na ina kiwango kikubwa cha sukari na asidi ambazo huzuia vijidudu wanaozaliana kwenye ngozi.
Tumia asali kwa kupaka wakati wa kuoga, kisha acha kwa muda na ioshe. Kufanya hivyo husaidia kuinawirisha ngozi.
Mayai pia ni muhimu kwa afya ya ngozi yako, kiini cha yai huwa na vitamini A na B, huku sehemu yenye ute ikiwa na protini nyingi ambayo ni muhimu pia kwa ngozi, ute wa yai ni muhimu katika kuifanya ngozi kuwa nyororo na yenye kung'aa na pia husaidia ngozi kujilinda vizuri na mionzi ya jua.
Matunda nayo ni muhimu pia hususani chungwa na limao ambayo husaidia kuimarisha afya ya ngozi, kwa sababu husaida kutengeneza collagen, ambayo ni aina ya protini inayotengeneza ngozi.
Ndani ya matunda hayo huwa na Vitamini C , ambayo husaidia sana kuondoa uvimbe na mikunjo ya ngozi na hivyo kuilinda ngozi isizeeke mapema.
Mboga za majani pia ni muhimu kwa afya ya ngozi kama tujuavyo zimesheheni vitamin na virutubisho vya aina mbalimbali vyenye faida kubwa kwa ngozi na mwili kwa ujumla. Mboga hizi za majani kwani husaidia ngozi kuzalisha seli mpya na kuondoa zile zilizokufa, hivyo kupunguza ukavu na kutunza ngozi na kuifanya ing’are na kuvutia.
Vyakula vya baharini kwa ujumla ni vizuri kwa afya ya ngozi. Vyakula vingi vya baharini vina kiwango kikubwa cha Zinc na Omega 3 ambazo ni muhimu kwa siha ya ngozi. Faida za Omega 3 ni pamoja na kuondoa kukakamaa au ukavu wa ngozi, kupunguza kuvimba na kukunjamana kwa ngozi na husaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini hivyo kuboresha ngozi.
Anza kupenda kula vyakula vyenye lishe bora kwa kuwa na ngozi bora zaidi.
Post a Comment
Post a Comment