Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro ametoa ufafanuzi kuhusu sakata la askari kufyatua risasi hewani mbele ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima na kusema Polisi walifanya vile ili kuwatia nguvuni watuhumiwa.
Kamanda Sirro amesema hayo pindi alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari ofisini kwake baada ya kuenea maneno sehemu mbalimbali zikidai polisi hao hawakutumia busara katika kufanya kazi yao.
“Kimsingi ninachosema ile bunduki tunayowapa askari ni kwaajili ya matumizi na tumewapa maelekezo..Kikubwa wananchi wajue suala la utie wa sheria bila ya shuruti ni la msingi, ukikataa kutii sheria tuna kila namna tunahakikisha tunakukamata na kukupeleka panapo husika. Kwa hiyo askari Polisi alichokifanya ni kutumia uzoefu wake, umakini wake kuhakikisha kwamba gari ambalo ni kielelezo, dereva ambaye ni mtuhumiwa na Mhe. Malima ambaye ni mtuhumiwa wanapelekwa vituo vya polisi na wamefanikisha hicho na leo amepelekwa mahakamani". Alisema Sirro
Katika hatua nyingine, Malima ameachiwa huru kwa dhamana ya Milioni tano baada ya jana kuweka kizuizini na kupandishwa Mahakamani kwa kosa la kumzuia askari kufanya kazi yake.
Post a Comment
Post a Comment