Utamaduni ni miongoni mwa mambo yanayotajwa kuhifadhi hadhi na heshima ya mtu na kumfanya atambulike kila mahali. Mbali na hayo, lakini zipo tamaduni ambazo zinabaki kuwa za sehemu moja pekee na haziwezi kusambaa sehemu nyingine.
1: Usiache kusalimia uwapo Ufaransa
Kila unapotembelea nchi ya Ufaransakumbuka kusalimia. Neno “Bonjour madame, monsieur” lazima liwe la mwanzo kutoka kinywani mwako, vinginevyo utachukuliwa kuwa unawadharau watu.
2: Usipige honi wakati unaendesha gari ukiwa Norway
Kama kuna jambo unalotakiwa kuwa makini uwapo Norway ni hili, kutopiga honi ukiwa unaendesha gari. Katika nchi ya Norway honi hutumika wakati wa dharura tu, hivyo kupiga kwako honi kutasababisha taharuki.
3: Usitumie mkono wa kushoto ukiwa India
Kwa mujibu wa utamaduni wa India ni kuwa mkono wa kushoto si salama. Hivyo jitahidi kila mara uwapo katika nchi hii kutumia mkono wa kulia kusalimia watu.
4: Usimalize chakula kwenye sahani ukiwa China
Nchini China, wageni waungwana hawamalizi chakula chote kwenye sahani. Kufanya hivyo hutafsiriwa mwenyeji wako hakukupa chakula cha kutosha. Sanjari na kubakisha chakula kwenye sahani, unaruhusiwa kubeua kama heshima kwa mpishi.
5: Usizungumze na mtu mikono ikiwa mfukoni uwapo Ujerumani
Unapanga kutembelea Ujerumani?Jihadhari na kuzungumza na mtu wakati mikono yako ikiwa mfukoni, kitendo hicho kuchukuliwa kama jeuri. Pia ni utamaduni wa nchi hiyo kuweka mikono juu ya meza wakati wa kula.
6: Marufuku kutabasamu mbele ya mgeni ukiwa Urusi
Upo usemi unaosema; “Tabasamu, na ulimwengu utatabasamu nawe”. Uwapo nchini Urusi usemi huu hauna maana yoyote. Warusi wanaona kutabasamu ni ishara ya karibu, ikionesha mshikamano baina yao. Kama utatabasamu mbele ya mgeni hukuchukulia kama mnafiki.
Post a Comment
Post a Comment