const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Baada ya miaka 118 Tottenham wanaondoka nyumbani kwa kuisulubu Man United. - HABARI MPYA

..

Baada ya miaka 118 Tottenham wanaondoka nyumbani kwa kuisulubu Man United.

Tottenham Hotspur wakiwa nyumbani waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Manchester United na kuuaga uwanja wao wa White Hart Lane kwa kishindo.

Ushindi huo wa Tottenham ni wa 17 katika uwanja huo kati ya mechi 19 walizocheza hapo huku wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja katika uwanja huo msimu huu.

Katika mechi hizo ni magoli 9 tu wameruhusu kufungwa wakiwa hapo huku michezo 12 wakiwa wamecheza bila kuruhusu goli na wakishinda mechi 14 mfululizo katika uwanja huo.

Mabao ya Tottenham yalifungwa na Victor Wanyama na Harry Kane ambaye hilo ndio lilikuwa bao lake la kwanza kuifunga Manchester United tangu aanze kuichezea Tottenham huku lile la Man United likiwekwa kimiani na Wayne Rooney.

Ushindi huo umeihakikishia Tottenham kumaliza katika nafasi ya pili ya ligi na kumfanya kocha wa Manchester City Pep Gurdiola kwa mara ya kwanza katika misimu nane iliyopita kumaliza ligi nje ya nafasi mbili za juu.

Huo ndio ulikuwa mchezo wa mwisho kwa Tottenham katika uwanja huo ambao wamekuwa hapo kwa miaka 118 na sasa watahamia katika uwanja wa Wembley huku wakisubiri uwanja mpya kukamilika katika msimu wa mwaka 2018/2019.

Related Posts

Post a Comment