Aliyekuwa Rais wa Korea Kusini, Park Geun-hye amefikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza kujibu mashtaka yanayomkabili, tangu alipokamatwa mwezi Machi mwaka huu.
Mwanasiasa huyo aliyeondolewa madarakani kwa kashfa nzito, anakabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwa ni pamoja na rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na kuvujisha siri za Serikali. Hata hivyo, Park aliyefikishwa mahakamani hapo na gari la magereza akiwa amefungwa pingu mikononi alikana mashtaka yote dhidi yake.
Park anatuhumiwa kushirikiana na rafiki yake, Choi Sonn-sil, kuchota fedha kinyume cha sheria kutoka kwa makampuni makubwa ya nchi hiyo ikiwa ni pamoja na kampuni ya Samsung, kwa malengo ya kupata mrejesho wa faida ya kisiasa.
Choi Soon-sil ambaye pia anakabiliwa na mashtaka alifikishwa mahakamani pamoja na mwanasiasa huyo lakini pia alikana mashtaka yote dhidi yake.
Kiwango cha juu zaidi cha adhabu kwa kosa la kupokea au kutoa rushwa nchini Korea Kusini ni kifungo cha maisha jela.
Post a Comment
Post a Comment