WANANCHI mjini Njombe wameiomba serikali kuboresha kituo cha mabasi cha Njombe Mjini wakati ikiendelea na ujenzi wa Kituo kipya cha mabasi ambacho Ujenzi wake bado unaendelea mkoani humo.
Kituo kinacho tumika kwa sasa kinajaa tope pindi mvua inaponyesha katika maeneo hayo na kusababisha kelo kwa wasafiri na wahudumu wa mabasi yanayoingia na kutoka katika mji wa Njombe kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya mkoa huo.
Wananchi hawa wanazungumza na starTv Mjini Njombe ambapo wanaomba halmshauri ya mji wa Njombe kuikarabati Stendi hii ya Mji wa Njombe ili kuwasaidia wanapo safiri wakikumbwe na kero ya Tope.
Hata hivyo baadhi ya madereva wanasema kuwa nauli zinaweza kupanda kutokana na ubovu huo kwa kuwa uharaibifu wa vyombo unakuwa mkubwa.
Kuhusu kukarabati stendi ya Njombe mjini ya sasa Mwenyekiti anasema kuwa haita karabatiwa kwa sababu kuna stendi mpya inajengwa huku zile barabara za vijijini kuwa imara.
Amesema kuwa stendi hiyo inapitia katika hatua mbalimbali na kuwa sasa inaingia katika hatua ya kujenga sakafu na wamechukua ushauri wa waziri mkuu walio washauri alipokuwa mkoani humo miezi kadhaa iliyo pita.
Waziri mkuu akiwa mkoani Njombe alimtaka mkandarasi huyo kujenga stendi hiyo katika eneo la Sakafu kwa kiwango imara.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI STENDI YA NJOMBE ILIVYO CHAFUKA KUKINYESHA..................
Post a Comment
Post a Comment