const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Sanchez awapa Arsenal sharti hili, laa sivyo ataenda Chelsea bure - HABARI MPYA

..

Sanchez awapa Arsenal sharti hili, laa sivyo ataenda Chelsea bure


  
3971
 
0
SHARE 
Arsenal na Sanchez bado ni vuta nkuvute, hakuna lolote walilokubaliana na hakuna upande wowote unaosema lolote, lakini ukweli ni kwamba Sanchez hajasaini mkataba mpya.
Lakini sasa tetesi mpya zinadai Sanchez ameamua kubaki katika klabu hiyo, Sanchez ambaye yuko katika rada za PSG na Chelsea anaonekana kama amelegeza moyo na kuamua kubaki na washika bunduki hao wa London.
Arsenal hawana uhakika wa kucheza UEFA msimu ujao kwani hadi sasa wako nafasi ya 5 lakini Sanchez anaonekana kama hajali hilo na yuko tayari kuitumikia Arsenal kwa msimu mmoja uliobaki.
Sanchez habaki Arsenal hivi hivi bali amewapa masharti Arsenal, inadaiwa Sanchez amewataka Arsenal kusajili majina makubwa katika usajili huu ili kuifanya timu hiyo iwe ya ushindani mkubwa katika msimu ujao wa ligi.
Endapo Arsenal watashindwa kufanya hivyo msimu huu baasi kuna hati hati kubwa ya Sanchez kuondoka bure Arsenal katika dirisha la mwakani la usajili kwani mkataba wake na Arsenal utakuwa umekwisha.
Arsenal walimuahidi Sanchez kiasi cha £250 000 kwa wiki lakini bado Mchile huyo ameweka ngumu kusaini kandarasi ya kuitumikia klabu hiyo ya London.
Arsenal wamekuwa na hulka ya kununja wachezaji ambao hawana majina makubwa kwa muda mrefu na hiyo imekuwa kati ya sababu zinazowafanya wahangaike kupambana na klabu kubwa kama Chelsea, Barcelona na timu za nje ya Uingereza.
Lakini sharti aliloipa Arsenal linaweza kuwafanya Arsenal kuwa klabu kubwa, wakati suala la Sanchez likikamilika, suala la Arsenal na Ozil bado nako hakijaeleweka.

Related Posts

There is no other posts in this category.

Post a Comment