const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Giggs amtaja mchezaji bora kuwahi kucheza naye - HABARI MPYA

..

Giggs amtaja mchezaji bora kuwahi kucheza naye

Ryan Giggs pengine ni kati ya wachezaji ambao wamecheza dhidi ya wachezaji wengi sana ulimwenguni, michezo zaidi ya 960 ndani ya misimu 24 inaonesha dhahiri jinsi Giggs alivyo nguli.
Amewahi kucheza na wachezaji wanaotajwa kuwa ni kati ya wachezaji bora sana kuwahi kutokea ulimwenguni, akiwemo Wayne Rooney, Ruud Van Niestroy, Roy Keane na hata Andy Cole.

Lakini kati ya hao wote Giggs ana mchezaji mmoja tu ambaye kwake anamuona kama alikuwa bora zaidi, Giggs anaona wote aliocheza nao ni bora na ndio maana walumsaidia kushinda vikombe vingi lakini yupo aliyewazidi wote.

“Mchezaji bora niliyecheza naye ni ngumu kumtaja kwakweli, lakini nadhani Cristiano Ronaldo ni bora sana” alisema Giggs wakati akihojiwa.

Cristiano ambaye kwa sasa ndio mchezaji mwenye tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa miaka 6 aliyoiyumikia Manchester United aliweza kubeba kombe la FA, kombe la Champions League, kombe la EPL na alifanikiwa kuchukua tuzo karibia zote ikiwemo Ballon d’or akiwa Uingereza.

Baada ya kuhamia Real Madrid kwa uhamisho uliovunja rekodi ya usajili kwa wakati huo wa £80m Ronaldo bado ameendelea kuweka rekodi na kuzidi kubeba makombe na hii inawafanya watu wengi duniani akiwemo Giggs kuamini Ronaldo ni bora.

Related Posts

Post a Comment