const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Kama ni Kweli Hili la Chuo cha DIT, Basi Watanzania wa Kudunduliza Wasahau Elimu ya Juu..!!! - HABARI MPYA

..

Kama ni Kweli Hili la Chuo cha DIT, Basi Watanzania wa Kudunduliza Wasahau Elimu ya Juu..!!!

nimepitia maeneo ya DIT kumwona mtoto wa rafiki yangu asomaye chuoni hapo akiwa mwaka wa kwanza. Mimemkuta kajiinamia kama anaongea peke yake. 

Nilivyomuuliza kulikoni kanijibu nina hati hati ya kurudia mwaka. Nikamuuliza umefeli? Akasema hapana,nmechelewa kumalizia ada ya chuo.


Nikamuuliza,umechelewa au hujalipa? Akaniambia hivi...wakati najoin mwaka jana,nililipa nusu kama ilivyokawaida ya wanachuo tunaokosa mikopo na nusu iliyobaki nmelipa juzi lakini wahasibu wamegoma kupokea bank slip kuwa hadi niende kwa registrar, nmeenda kwa registrar kasema hawezi tena kuruhusu isipokuwa nirudie mwaka! Nikabaki nashangaa. 

Hivi mtu amelipa tayari pesa iko ndani ya akaunti ya chuo,anaambiwa arudie mwaka kisa kachelewa kulipa kwa wiki mbili!!! Sio kuwa mwaka umeisha na wala si kama ni wakati wa mitihani kazuiwa hadi alipe bali kachelewa kulipa na sio kwamba hajalipa! 

Sasa binafsi nmebaki nimeduwaa, hivi watanzania kwa pesa yetu ya kudunduliza mzazi kajichanga, kanyimwa mkopo amejibana akakamilisha bado tena mtoto anapata frustrations za kurudishwa aanze tena upya!!??

Nimejiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu! Hii ni kumkomoa au kumsaidia? Hii itakuwa ndo kumsaidia mtoto wa mtanzania apate elimu ya juu au wanaotakiwa wasome ni wale watakaopata mikopo na watoto wa matajiri tu?

Kabisa nimekosa majibu na nimeishia kumshauri akamuone mkuu wa chuo labda hajaelewa kilichosemwa maana itakuwa hatari.

Related Posts

Post a Comment