Kama ilivyozoeleka watu wengi tuna video, picha au vitu ambavyo tumeweka kwenye smartphone zetu, ambavyo si vizuri vikaonekana kwa kila mtu. Tatizo la smartphone ni kwamba kila mshikaji utaekutana nae juma au saidi atataka aangalie muundo, uwezo, kamera na toleo lake. Na inakuwa vigumu kuweza kumkatalia mtu hasa kama ni rafiki yako wa karibu sana.
Ukisema utengeneze folda ambalo linaonekana kwa urahisi halafu uweke picha, video na faili zako za siri lazima watashitukia na kutambua kilichomo ndani. Siku za nyuma , tulikuwa tunatengeneza folda halafu tunaliandika 'virus' na kuweka vitu vya siri humo ili kumtisha mtu asiweze kufungua kutokana na jina la folda hilo akizani ni kirusi kweli. Ila siku hizi ujanja huu kila mtu anaujua. Wakati kukiwa na njia nyingi tu za kuweza kuficha vitu vyako vya siri kwenye smartphone yako, leo nitakuonesha namna ya kuficha vitu vyako vya siri katika App unayoitumia kila siku ya Calculator.
Ndiyo, Calculator! kuna app inayoitwa 'Smart Hide Calculator' ambayo unaweza ukaitumia kukokotoa mahesabu pia inaweza tumika kuficha vitu vyako vya siri na muhimu kwa watu wadukuzi wa mambo. Smart Hide Calculator ni app ambayo unaweza ukahifadhi picha, video na faili zako muhimu kwa siri kwenye mgongo wa Calculator. Unachotakiwa ni kuweka namba ya siri kisha unabonyeza sawa sawa '=' kisha vitu vyako vitaonekana ndani ya app hiyo.
Fuata hatua zifuatazo kuweza kutumia app hiyo.
Hatua ya 1. Kwanza kabisa, pakua kisha ingiza app ya Smart Hide Calculator kwenye Google Playstore au bonyeza link ifuatayo >> Pakua hapa Smart Hide Calculator
Pakua 'Smart Hide Calculator' Playstore
Hatua ya 2. Fungua App yako itakutaka uingize namba ya siri. Hakikisha kuweka namba ya siri ambayo ni ngumu kwa mtu kuweza kuitambua na rahisi kwa wewe kuikumbuka kwa sababu hiyo ndiyo itatumika kufungua na kufungia vitu vyako vya siri ndani ya calculator hiyo.
Ingiza namba ya siri
Hatua ya 3. Baada ya kuhakiki namba ya siri, wewe na mtu yeyote atakayefungua simu yako ataiona app hiyo kama calculator ya kawaida kabisa.
Muonekano wa Calculator hiyo
Hatua ya 4. Ili kuingiza vitu vyako vya siri, unatakiwa kuingiza namba yako ya siri kisha bonyeza kitufe cha sawa sawa '=' ili kufungua vitu vya ndani.
Fungua vitu vyako vya ndani ya app hiyo
Hatua ya 5. Baada ya kufunguka ndani utaona mipangilio ya kuficha mafaili (Hide Files), kuyaondoa mafichoni (Unhide Files), kubadili namba ya siri (Change Password) nakadhalika.
Muonekano wa ndani wa app hiyo
Bonyeza kwenye 'Hide Files' kisha chagua mahali ulipo hifadhi vitu vyako kama video, picha, miziki au faili unazotaka kuzificha.
Chagua mahali ulipoweka vitu vyako
Bonyeza 'OK' kuficha vitu vyako muhimu ndani ya app inayoaminika duniani, Calculator yako. Kama ukitaka kuyafichua mafaili yako fungua hiyo Calculator kisha chagua 'Unhide Files' na faili zako zitakuwa nje ya Calculator hiyo.
Bonyeza kwenye 'Unhide Files' kufichua vitu vyako
Kama ukisahau namba ya siri, usijali, unaweza ukairudisha namba yako ya siri kwa kuandika namba hizi 123456789+987654321
Namba ambazo zitakusaidia kama ukisahau namba yako ya siri
App ya Smart Hide Calculator kiufupi ni moja kati ya app nzuri kwa kuficha faili na vitu vyako muhimu kwenye smartphone yako.
Post a Comment
Post a Comment