const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Ehe..Umesikia Hii ya Rais wa Somalia Kutangaza Siku za Kuwasamehe Al Shabaab..? - HABARI MPYA

..

Ehe..Umesikia Hii ya Rais wa Somalia Kutangaza Siku za Kuwasamehe Al Shabaab..?

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi “Farmajo” ametoa msamaha wa siku 60 kwa wanamgambo wa kundi la Al-Shabaab akiwataka kujisalimisha ii waweze kupatiwa mafunzo, elimu na ajira.

Kwa mujibu wa BBC, siku 60 zikiisha bila ya wanamgambo hao kujisalimisha itakuwa ni sawa na kutangaza vita dhidi ya kundi la hilo.


Hatua hii inakuja baada ya shambulizi la kujitoa mhanga kutokea karibu na jengo moja la Serikali Mjini Mogadishu ambapo watu 7 waliuawa pamoja na msururu wa utekaji nyara kwa wafanyakazi wa kutoa misaada katika taifa hilo linalokumbwa na ukame.

Mashambulizi yamekuwa ya mara kwa mara na vikosi vyote nchini Somalia vimekuwa katika hali ya tahadhari ili kukabiliana na tishio lolote kwa usalama.

Aidha, amesema kuwa amefanya mabadiliko kwa maafisa wa vyeo vya juu katika Idara ya Ujasusi na Polisi ili kujiandaa kwa vita dhidi ya al-Shabab.

Related Posts

Post a Comment