const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); USINGIZI WA MUUGUZI WASABABISHA KIFO CHA MTOTO - HABARI MPYA

..

USINGIZI WA MUUGUZI WASABABISHA KIFO CHA MTOTO

Wananchi wa kijiji cha Bugulula, wilayani Geita, jana wamefanya jaribio la kutaka kuchoma moto zahanati kijijini hapo baada ya muuguzi wa zamu, Andulalie Donald kudaiwa kukataa kuamka usiku kumzalisha mjamzito na kusababisha kifo cha mtoto.
Hata hivyo Andulalie alisema “sijasikia nikiamshwa usiku, hata aliyekuja saa 12 alfajiri alinigongea nikaamka na kumzalisha, nilipoona mtoto ana shida niliita gari aende Geita. Hayo malalamiko ya wananchi sikuyasikia”

Awali ilidaiwa saa saba usiku kuamkia machi 15, mjamzito Esther Elias alifikishwa katika zahanati hiyo na kumgongea muuguzi lakini hakuamka.

Wakizungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi aliyefika kuwatuliza wananchi hao, Maza shabiko, ambaye ni mkwe wa Esther alidai kuwa walipofika zahanati hakuna muhudumu aliyeamka, na baada ya Esther kulalama kuwa anahisi uchungu ilibidi wamzalishe nje kwenye mchanga huku kukiwa na giza.

Alisema baada ya kujifungua tumbo lilibaki kubwa huku akilalamika kuwa na uchungu zaidi, hivyo walikwenda kumgongea muuguzi lakini hakuna aliyeamka hadi saa 11 alfajiri alipotoka mtoto wa pili akiwa amechoka na baadaye kufariki dunia.

Hata hivyo, Kapufi alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Ali Kidwaka, kuwachukulia hatua za kinidhamu wauguzi wanne wa zahanati hiyo waliosababisha vifo hivyo.


Related Posts

Post a Comment