Kocha mkuu wa Madini FC Abdallah Juma ametoa ufafanuzi wa kina kuhusu tetesi za usajili zilizoibuka kuhusu mchezaji wake Awesu Awesu kuhusishwa na mpango wa kusajiliwa na klabu ya Simba baada ya kuonekana akizungumza na mwenyekiti wa kamati ya Usajili Zacharia Hans Poppe mara baada ya mchezo wa hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho hapo jijini Arusha.
Abdallah Juma amesema kiongozi huyo wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo, ni kweli alifanya mazungumzo na mchezaji wake na wamempa nafasi ya kuwasilisha ofa mezani endapo ana nia ya dhati ya kumsajili.
Hata hivyo kocha huyo amesema mipango mingine ya usajili wa mchezaji huyo kama itatokea ipo katika mamlaka za uongozi wa juu wa klabu ya Madini FC japo anatambua Awesu ana uwezo wa kucheza katika klabu yoyote hapa nchini.
“Najua suala hilo lipo lakini mimi siwezi kulizungumzia rasmi, wamesema wanataka kukutana na mchezaji pamoja na viongozi kwa hiyo hilo suala litakuwa na utawala lakini hata mimi najua.”
“Kupitia radioni wamesema walifanya mazungumzo na mchezaji na kikubwa alikuwa anataka mawasiliano, atazungumza nae na atazungumza na uongozi wakikubaliana basi atakwenda kufanya kazi huko.”
Awesu Awesu alishawahi kuwa Azam FC kipindi cha nyuma akicheza kwenye kikosi cha U20 lakini baadae akajiunga na Madini FC ambako yupo hadi sasa.
KAMA ULIMIS VIDEO YA MCHEZAJI WA Ghana ALIE JIKANYAGA KWA KUWASHUKURU MUKE NA MCHEPUKO WAKE TAZAMA HAPA
Post a Comment
Post a Comment