Tarehe rasmi ya ndoa kati ya mchezaji bora wa dunia mara 5 Lioneil Messi na mpenzi wake wa muda mrefu Antonella Ruccuzo haijatangazwa rasmi,lakini imefahamika kwamba ndoa hiyo imekaribia.
Harusi kati ya Lioneil Messi itakuwa sherehe mbili,moja ikifanyika nchini Hispania kwa ajili ya wachezaji na watu wa karibu wa Messi nchini humo, na nyingine ikifanyika Argentina ikiwa maalum kwa ajili ya marafiki wa Messi na Antonella.
Tayari watu mbalimbali maarufu wameshapewa mualiko katika sherehe hiyo, lakini jambo la ajabu ni kwamba beki wa kati wa Barcelona Gerald Pique na mpenzi wake Shakira wanaweza kutoswa katika sherehe hiyo.
Kama ilivyo kwa wachezaji wengine, Lioneil Messi na Gerald Pique ni marafiki lakini tatizo ni kati ya mke mtarajiwa wa Messi bibie Antonella na mpenzi wa Gerald Pique mwanamuziki Shakira.
Shakira na Antonella hawana uhusiano mzuri kwani toka mwaka 2010 hawajawahi kukutana na kuongea. Na vyanzo vya habari vinasema Antonella hampendi hata kidogo wifi yake huyo na sababu imefahamika.
Imefahamika kwamba Antonella ana urafiki wa karibu sana na mpenzi wa zamani wa Pique aitwaye aitwaye Nuria Thomas. Antonella alichukizwa sana na kitendo cha Pique kuwa na Shakira na kumuacha Nuria.
Na sasa Antonella ameamua kumuonesha wazi wazi Shakira chuki dhidi yake. Ripoti zinadai Antonella amekataa kata kata Shakira kupewa mualiko katika harusi yake,na kwa maana hiyo familia nzima ya Shakira akiwemo mumewe na watoto wao watakosa sherehe hizo.
KAMA ULIMIS VIDEO YA MCHEZAJI WA Ghana ALIE JIKANYAGA KWA KUWASHUKURU MUKE NA MCHEPUKO WAKE TAZAMA HAPA
Post a Comment
Post a Comment