Rais wa Brazil Michel Temer ameahama katika Ikulu ya nchi hiyo (Alvorada Palace) kwa kile alichoeleza kuwa ni kutokujisikia vizuri pamoja na kuona mizimu inayomfanya ashindwe kulala usiku.
Ikulu ya Rais wa Brazil
Kiongozi huyo pamoja na mke wake, Marcela (33) wameyahama makazi hayo rasmi kwa kile walichoeleza vyombo vya habari kutokujisikia hali ya kawaida na kuona vitu vya ajabu ajabu vinavyowafanya washindwe kulala usiku na kusema huenda ikawa ni mizimu.
Rais na mkewe baada ya kuhama katika makazi hayo, wamerejea katika makazi yao ya awali (Jaburu Palace) alipokuwa akiishi wakati akiwa Makamu wa Rais chini ya uongozi wa Rais Dilma Rousseff aliyeondolewa madarakani mwaka 2016 kwa makosa ya rushwa.
Jengo la makazi ya Makamu wa Rais wa Brazil
Tukio hili la Rais kuhama makazi yake limekuja wakati ambao nchi hiyo ina mgogoro mkubwa wa kisiasa kufuatia tuhuma za rushwa zinazowakumba viongozi wengi wa kisiasa pamoja na taasisi za serikali.
Post a Comment
Post a Comment