const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Rais Magufuli ni zawadi kutoka kwa Mungu inawezekana usielewe lakini ipo siku utaelewa- Makonda - HABARI MPYA

..

Rais Magufuli ni zawadi kutoka kwa Mungu inawezekana usielewe lakini ipo siku utaelewa- Makonda


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa Rais Magufuli kuwa ni zawadi kutoka kwa Mungu huku akisema kuwa watu inawezekana wasielewe lakini ipo siku moja wataelewa.


Alitoa kauli hiyo Jumatano hii wakati akizungumza na wadau mbalimbali waliohudhuria hafla yake ya kutimiza mwaka mmoja tangu awe mkuu wa mkoa huo.

Alisema “Naomba nifunge kwa kumshukuru Rais Joseph Pombe Magufuli ni zawadi kutoka kwa Mungu, Rais Magufuli ni zawadi kutoka kwa Mungu inawezekana usielewe lakini kuna siku moja utaelewa na mara nyingi watu tunaopewa na Mungu huwa hatuwaelewi mpaka wanapomaliza muda wao ndiyo tunaanza kusema eeh hivi kumbe alikuwa na kusudio jema, kwasababu kuja kuelewa kuwa alikuwa na kusudio jema kuelewa inachukua muda , lakini mimi naamini Rais wetu ni zawadi kutoka kwa Mungu.”

“Rais ambaye hana kitu ambacho anakificha moyoni anakwambia ukweli unaokuhusu wewe , hakuchekei pale unapomuudhi na ameamua kunyima na serikali yake kwaajili ya wananchi unataka Mungu akufanyie nini tena ,Dar es salaam mna taka Mungu awafanyie nini tena. Ukiona wale wanaosema ooh Rais jua tu wameguswa maslahi yao kwahiyo watu walizoea kula kula kwahiyo wakishakanyagwa kule wanapiga kelele,” aliongeza Makonda.

Related Posts

Post a Comment